eGotickets Search

Filter events and get the results you need

GFC 2017 Great Lake Global Summit Dodoma, Tanzania

By Global Faith Coalition
Wed, Sep 20 7:00AM - Sun, Sep 24 5:00PM
University of Dodoma, Dodoma

GLOBAL FAITH COALITION INAKULETEA 2017 GREAT LAKE GLOBAL SUMMIT JUU YA KANISA LA KARNE YA 21 DODOMA, TANZANIA NDIKO WOTE WANAKOELEKEA. (TAREHE 20 – 24/ SEPTEMBA) Hotlines: 0783 919 745, 0652 101 863, 0754 808976 Ni kusanyiko la karne linalowaleta pamoja wageni wa kitaifa na kimataifa kutoka ulimwengu mzima, kama vile Marekeni, Uingereza, India, Ubelgiji, Israeli, Cameroon, Nigeria, Zambia, Afrika kusini, Uganda, Kenya, Zimbabwe, Rwanda, Malawi, Botswana, Liberia, Ghana, Sierra Leone na nyinginezo, kwa ajili ya siku 4 za ushirika wa Neno juu ya Neno kuu “KANISA LA KARNE YA 21” Siku zote kuna Baraka kuu wakati wana wa Mungu kutoka ulimwenguni mzima wanapokusanyika pamoja katika Ushirika ili kupokea mipauko mipya kutoka katika moyo wa Mungu. Kusanyiko hili la ulimwerngu na ushirika litaishia Dodoma, mji mkuu mpya wa Tanzania. Walio na maswali na kiu ya kumjua Mungu, wahubiri wa injili na waamini kutoka ulimwengu mzima watakusanyika katika CHUO KIKUU CHA DODOMA UDOM, tarehe 20 – 24/Septemba ili kuitafuta nia ya Mungu juu ya maeneo makuu na masomo juu ya kanisa la karne ya 21. Pia kufanya ushirika mbadala ili kuuendeleza ufalme wa Mungu Ulimwengu mzima. Itakuwa ni fursa ya kipekee kwa watu wenye maono ya Mungu kwa ajili ya karne ya 21, wana takinolojia, wana mikakati, wenye mipango madhubuti, wenye fikra, viongozi masokoni, wahubiri wa injili, mabalozi wa ulimwengu na raia wa ufalme, wote watakutana kwa siku nne katika ushirika nuruni. Kutakuwepo na warsha mbalimbali kla siku na kuhitimishwa na kusanyiko la wote wakati wa jioni. MASOMO YATAKAYOFUNDISHWA NI PAMOJA NA 1. Kuisindania Imani. 2. Kuzirudisha tena huduma kuu tano katika kanisa la Karne ya 21. 3. Kanisa la karne ya 21. 4. Mitazamo ya kinabii juu ya mwenendo wa Mungu leo. 5. Kuishinda vita ya uchumi (Mpango wa Mungu wa kiuchumi kwa ajili ya kanisa la karne ya 21). 6. Mkakati wa huduma kwa ulimwengu kwa karne ya 21. 7. Huduma mahali penye soko katika karne ya 21. 8. Wajibu wa kanisa juu mabadiliko ya kitaifa, maendeleo ya kijamii na katika kutatua changamoto za ulimwengu. 9. Huduma ya mvinyo mpya ya roho Mtakatifu. 10. Kuzitambua nyakati/ Bibi harusi wa kristo. Hili ni tukio la lazima kulihudhuria hasa kwa waamini na viongozi wa kikristo wenye kumaanisha na waliojitoa. Unaweza kuwasiliana nasi ili kupata maelezo juu ya kujiandikisha ili uweze kuhudhuria. E-mail: globalfaithcoalition@yahoo.com Simu 1. 0783 919 745 2. 0652 101 863 3. 0754 808976 Askofu Mgaya Global Faith Coalition ni Taasisi ya kikristo isiyojiendesha kwa faida na ni umoja wa viongozi wa kikristo Ulimwenguni unaoundwa na watu wa matabaka mbalimbali, wenye lengo la kurejesha Imani, waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu, ili kuliandaa na kuliwezesha kanisa la Karne ya 21. Website: http:llglobalfaithcoalition. Ofisi za kimataifa: 6383 Deshong Dr - Lithonia, Georgia, USA - Biyemassi Yaounga, Cameroon. Rais Global Faith Coalition: Dr. Benard Etta Tel + 1-240-356-3010/ +255758 297136

Google Map