VMV Book Review Tea Party (Mapitio ya Kitabu)

VMV Book Review Tea Party (Mapitio ya Kitabu)
past about 2 years ago

Sat, Apr 23. 5:30AM - 8:30AM

Dar es Salaam, Tanzania Dar es Salaam, Tanzania

Event Details

Kama mwandishi, huwa nina hamu ya kujua maoni ya wasomaji kuhusu kitabu changu. Nawashukuru kwa lolote wanalosema baada ya kusoma na kutafakari yaliyomo kitabuni. Kama kitabu kimewaridhisha au kuwafurahisha, nami nafurahi. Wakiona dosari wakazibainisha, nitawashukuru kwa kunielimisha na kunipa nafasi ya kujiboresha katika kazi yangu ya uandishi wa vitabu.

Napenda kuwakaribisha watu ambao wameshasoma kitabu cha simulizi ya "Vipande vya Maisha Vilivyopotea" chote kwa ajili ya kufanya mapitio siku ya 23/04/2016 - World Reading Day. Upitiaji wa kitabu hiki utafanyikia hapa jijini Dar es Salaam. Nafasi ni chache kwa ajili ya wasomaji wa kawaida kwani nafasi nyingine zimeenda kwa wadau wengine wa usomaji wa vitabu kama vile Wahariri wa vitabu, Wakufunzi wa vyuo mbalimbali, Wahariri wa magazeti, nk.

Naomba uthibitishe ushiriki wako mapema iwezekanavyo